Wizara ya Maliasili na Utalii, inatumia Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), maarufu Sabasaba kuhamasisha utalii wa ndani, ikiwamo mashindano ya AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwaka ujao.
Akizungumza katika maonesho hayo, Ofisa Utalii Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Naomi Mbilinyi, amesema wananchi wanapata elimu kuhusu fursa mbalimbali za utalii, ikiwemo uwekezaji, kuanzisha kampuni za utalii, kushiriki maonesho ya kimataifa na kutembelea vivutio vilivyopo nchini.
Mbilinyi amesema wanatoa elimu kuhusu fursa zitakazotokana na AFCON, likiwahamasisha watoa huduma za malazi, usafiri na sekta nyingine kujiandaa kupokea wageni wengi watakaofika nchini wakati wa mashindano hayo.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED