Bianca kumtetea Kanye West

By Moshi Lusonzo , Nipashe
Published at 01:11 PM Aug 14 2026
Bianca kumtetea Kanye West
Mtandao
Bianca kumtetea Kanye West

BIANCA Censori, ambaye ni mke wa rapa maarufu wa Marekani, Kanye West, huenda akalazimika kufika mahakamani kutoa ushahidi

BIANCA Censori, ambaye ni mke wa rapa maarufu wa Marekani, Kanye West, huenda akalazimika kufika mahakamani kutoa ushahidi katika moja ya kesi zinazomkabili mumewe.

Kwa mujibu wa TMZ, Bianca ni miongoni mwa mashahidi 22 ambao upande wa utetezi wa Kanye West umeorodhesha kuwa wanaweza kuitwa kutoa ushahidi katika kesi inayotarajiwa kuanza kusikilizwa mwezi Oktoba.

Kesi hiyo imefunguliwa dhidi ya Kanye na kampuni yake ya mavazi ya Yeezy, ikihusiana na madai ya mazingira mabaya ya kazi na namna aliyodaiwa kutendewa mlinzi wa usalama wa Donda Academy, Benjamin Provo.

Mbali na Bianca Censori, Kanye West mwenyewe pia ametajwa kuwa mmoja wa mashahidi wanaoweza kuitwa mahakamani kutoa ushahidi katika kesi hiyo.