Nicole hakufikiria mabaya

By Moshi Lusonzo , Nipashe
Published at 01:22 PM Aug 14 2026
Nicole Kidman
Mtandao
Nicole Kidman

MSANII maarufu wa filamu za Hollywood, Nicole Kidman, amesema ndoa yake na mwigizaji mwenzake, Tom Cruise, ilionekana kuwa jambo la kawaida

MSANII maarufu wa filamu za Hollywood, Nicole Kidman, amesema ndoa yake na mwigizaji mwenzake, Tom Cruise, ilionekana kuwa jambo la kawaida kwake wakati huo, licha ya kuonywa na baadhi ya watu wasifunge ndoa.

Kidman alisema wakati huo alikuwa akimpenda Cruise kiasi kwamba alikuwa tayari hata kuacha kazi yake ya uigizaji iwapo kufanya hivyo kungemwezesha kuwa naye.

Kwa mujibu wa mwanasanii huyo, uamuzi wa kuingia katika ndoa hiyo ulimjia kwa namna ya kawaida na hakuhisi kuwa alikuwa akifanya jambo lisilo sahihi, licha ya watu waliokuwa karibu naye kumshauri kutofanya hivyo.

Kidman na Cruise walioana mwaka 1990 baada ya kukutana wakati wakifanya kazi kwenye filamuDays of Thunder. Wawili hao walidumu katika ndoa kwa takribani miaka 11 kabla ya kutengana mwaka 2001.