KAMATI Kuu ya Chama cha National League for Democracy (NLD) imefanya kikao chake na kutoa maazimio kadhaa kuhusu uchaguzi Mkuu wa 2025 ambapo imeazimia kuunda Tume Maalum ya Tathimini ya Uchaguzi huo ndani ya siku 14.
Katibu Mkuu wa NLD,Doyo Hassan Doyo, katika taarifa yake aliyoitoa leo kwa vyombo vya habari baada ya Kamati Kuu kukutana kwa siku mbili kuanzia Julai 1 hadi 2,mwaka huu, amesema Kamati hiyo pamoja na mambo mengine itafanya kazi ya kuchambua matokeo ya uchaguzi wa rais,wabunge na madiwani.
Amesema kazi nyingine itakayofanywa na Kamati ya Kutathimini Uchaguzi Mkuu wa 2025, ni kutathimini mikakati ya kampeni iliyotumika pamoja na changamoto zilizojitokeza na kutoa mapendekezo maboresho yatakayokiwezesha chama kufanya vizuri katika chaguzi zijazo.
Kamati Kuu pia imeazimia kuwa viongozi wakuu wa chama waanze ziara rasmi katika mikoa yote kwa lengo la kuwashukru wananchi na wanachama waliokiunga mkono chama hicho wakati wa uchaguzi Mkuu wa 2025.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED