MWIGIZAJI wa Marekani, Jenna Ortega, amesema alipitia changamoto kubwa akiwa mwigizaji mtoto ili kuthibitisha kuwa anastahili kupewa nafasi za kuigiza katika filamu.
Jenna, mwenye umri wa miaka 23, alisema wakati mwingine alikaa siku nzima bila kula wala kunywa, akiamini kufanya hivyo kungemsaidia kuonyesha kuwa alikuwa anajituma.
Akizungumza na jarida laEsquirekuhusu miaka yake ya mwanzo katika tasnia hiyo, alisema alijikuta akijisukuma kupita kiasi ili kuthibitisha uwezo na thamani yake akiwa bado mtoto.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED