Mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa vikundi vya wilaya ya Mafia imebadilisha maisha ya wanufaika katika kujikwamua kiuchumi.
Utoaji wa mikopo hiyo kwa vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu ni utekelezaji wa Sera, Mikakati na Mipango ya Taifa ya kupunguza umasikini inayojumuisha Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050, Sera ya Maendeleo ya Jinsia ya mwaka 2023.
Pia Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007, Sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya mwaka 2004, Sera ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2004 pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2025-2030.
Makala hii Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mafia inaangazia kwa kina mafanikio ya serikali kupitia mpango huu muhimu kwa wananchi.
Utekelezaji na Ufadhili Endelevu.
Halmashauri ya Wilaya ya Mafia inatekeleza Sheria ya fedha za Serikali za Mitaa Sura ya 290 kifungu cha 37A kilichoweka utaratibu wa kutenga fedha za mapato ya ndani ya vyanzo visivyo lindwa vya mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya utoaji wa mikopo ya asilimia kumi.
Katika kipindi cha mwezi Februari 2025 hadi Machi, 2026 Halmashauri ya Wilaya ya Mafia imefanikiwa kutoa Sh.Bilion 1.88 kwa Vikundi 129 vya Wanawake ,
Vijana na Wenye Ulemavu.
Vikundi vya Wanawake 88 vimepatiwa sh.Milion 635.5, wakati vikundi 29 vya Vijana 29 vikinufaika na sh Milion 358.5 na wenye Ulemavu 12 wakipatiwa sh. Milion 94.
Mafia ilivyojikita kukuza Uchumi wa Vikundi Maalum
Kupitia mwongozo wa serikali, mikopo hii inagawanywa katika makundi matatu muhimu kwa uwiano ambayo ni Wanawake ambao wanapata asilimia 4 na wamekuwa mstari mbele kujiunga katika vikundi na kupokea mikopo hii kwa ajili ya biashara ndogo na za kati, uvuvi mdogo, na usindikaji wa mazao ya bahari.
Kundi la Vijana ambao mgawo wao ni asilimia 4 na wengi wamejiajiri kwenye sekta ya kilimo, ufugaji, usafirishaji, na ufundi kupitia mitaji hiyo.
Kadhalika Watu wenye Ulemavu wao wanapata asilimia 2 kundi hili limewezeshwa kuanzisha miradi midogomidogo inayowapa uhuru wa kiuchumi na kupunguza utegemezi.
Kuondoa Utengamano wa Kifedha Mafanikio makubwa ya serikali ni kuondoa changamoto ya ukosefu wa mitaji na kuwakomboa wananchi wa Mafia kutoka kwenye mikopo yenye riba kubwa na masharti magumu.
Mfumo huu wa mikopo isiyo na riba umewezesha miradi ya walengwa kukua kwa haraka na wao kuimarika kiuchumi.
Usimamizi na Ufuatiliaji Imara
Ili kuhakikisha fedha zinarejeshwa na kuwanufaisha wananchi wengi zaidi kama mfuko unaozunguka, Halmashauri ya Wilaya ya Mafia kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imekuwa ikitoa mafunzo ya usimamizi wa fedha, uandishi wa miradi, na mikataba.
Utaratibu huu umekuwa unasaidia vikundi kuelewa misingi ya biashara na kuepuka matumizi mabaya ya fedha.
Mtazamo wa Baadae
Serikali inafanya maboresho endelevu katika mfumo wa utoaji na usimamizi wa fedha hizi kupitia mifumo ya kielektroniki ili kuongeza uwazi na kupunguza changamoto zilizojitokeza huko nyuma.
Pia kumekuwa na mafanikio yaliyopatikana kwa Upande wa Wanufaika ambayo ni pamoja na ongezeko la kipato kwa makundi ya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu na hivyo kuchangia katika kukuza pato la Taifa.
Wanavikundi wamefanikiwa kupata mikopo midogomidogo na kati

M a f u n z o w a n a y o p a t i w a ni pamoja na ya Ujasiliamali, uongozi, utunzaji wa kumbukumbu, u m u h i m u w a ku we k a a k i b a , utatuzi wa migogoro katika vikundi, namna ya kujikinga na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na yasiyo ambukiza, lishe na udhibiti wa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Hali ya vikundi vinavyonufaika na mikopo imezidi kubadilika siku hadi siku na kwa kufanikiwa kumiliki mali baada ya kumaliza mikopo ambazo ni pikipiki, boti, mashine za boti.
Wanavikundi wameweza kuwa na uhakika wa kipato na ajira 903 zimeongezeka miongoni mwa makundi ya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu na hivyo kuimarisha uhakika wa chakula na kuboresha makazi.
Utoaji wa mikopo hiyo unaunga mkono mafanikio ya Mkoa wa Pwani katika uwezeshaji wa wanachi wa wilaya ya Mafia.
Kwa upande wa Utalii.
Wilaya ya Mafia ni moja ya wilaya katika Mkoa wa Pwani ambayo ina vivutio vingi vya utalii vilivyopo nchi kavu na ndani ya maji (baharini).
Katika kisiwa cha Mafia msimu wa utalii huanza mwezi Julai na kuisha mwezi wa Aprili wa mwaka unaofuatia kila mwaka.
Asilimia kubwa ya wageni hufika Mafia kutalii kwasababu ya uwepo wa samaki mkubwa na wa kuvutia Papa Potwe (Whale shark), magofu ya kihistoria pamoja na vivutio vya baharini kwa ajili ya utalii wa kuzamia/ kuogelea na kujifunza.
Katika mwaka 2024/25 kwenye eneo la Utalii, Wilaya ya Mafia imepiga hatua kubwa katika mambo mbalimbali ikiwemo kushiriki maonesho ya nanenane ambayo yalitumika kutangaza utalii wa kisiwa hicho kwa kusambaza vipeperushi.
Pia walitangaza utalii kwa kuonesha mkanda wa video,kufanya tamasha la utalii (Mafia Island Festival) ambayo ilikua chachu katika kuutangaza utalii wa kisiwa hicho.
Jambo lingine ni pamoja na Kushiriki maonesho ya biashara, viwanda na uwekezaji yaliyofanyika Kibaha ambapo vivutio vy a utalii wa Mafia vilitangazwa kupitia mkanda wa video na vipeperushi.
Vile vile upo ushirikishwaji wa wadau kwenye vikao vinavyohusu utalii ambapo tayari vikao vinne vimefanyika.
Njia nyingine ya iliyotumika kutangaza utalii wa kisiwa cha Mafia , Halmashauri kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii nchini (TTB) na Safari Chanel imeendelea kurusha matangazo kwenye usafiri wa SGR kwa njia ya video , pamoja na kwa vipindi mbalimbali vinavyorushwa na chaneli hiyo.
Katika msimu wa utalii 2024/25 Halmashauri kwa kushirikiana na wadau wa utalii imefanikiwa kutoa mafunzo ya utalii kwa vijana 16 wanaojihusisha na shughuli za utoaji wa huduma kwa watalii hotelini na kuwaongoza.
Pia kisiwa cha Mafia kimefanya ubunifu kwenye swala la utalii kwa kuvutia watalii kisiwani humo kama vile kuanzisha vikundi vya utalii wa kitamaduni kama upishi wa vyakula vya asili,sanaa za mikono na ngoma katika vijiji vya Kilindoni, Kiegeani,Juani na Dongo.
Utekelezaji wa malengo umefanyika kwa kukusanya kiasi cha sh. Milioni 107,105,000 ambayo ni sawa na asilimia 97.4.
Mapato hayo yanajumuisha malipo ya vibali vya kufanya utalii wa Papa Potwe ambao ni Sh. 120,000 pamoja na ushuru wa Halmashauri Sh. 106,985,000.
Hata hivyo mapato ya utalii wa Papa Potwe yamepungua kwa asilimia 11.5 ukilinganisha na mapato ya msimu wa 2023/2024 kutokana na sababu za asili ambazo ni athari za kimbunga hidaya.
Katika msimu wote wa utalii 2024/25 watalii 4,582 walitembelea kivutio cha utalii wa Papa Potwe na kati ya hao 157 ni watalii wa ndani ya Tanzania na 4,425 watalii kutoka nchi za nje.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED