Wilaya ya Kisarawe ni kati ya wilaya saba na Halmashauri tisa za mkoa wa Pwani na imekuwa ikikua kwa kasi kutokana na kutokana na ongezeko la watu.
Kwa mujibu wa takwimu ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, idadi ya watu ni 159.226 ambapo kati ya hao wanaume ni 79892 na Wanawake ni 79,334.
Wilaya hiyo inaendelea na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo inalenga kuleta maendeleo kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita kuanzia Julai 2025 hadi Septemba 2025 shughuli mbalimbali zimetekelezwa katika sekta ya Elimu, Afya, Maji, Kilimo na ushirika, Viwanda na Biashara , Mifugo, Maliasili na Utalii, Utawala bora, Nishati, Usafirishaji na Uchukuzi.
Kisarawe inavyojivunia utekelezaji wa miradi ya Maendeleo
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa mwaka wa Fedha 2025/26 iliidhinishiwa Jumla ya kiasi cha Sh.1Bilion 12.6 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na shughuli za maendeleo ambapo fedha za Mapato ya ndani ni Sh. Bilion 1.5, Ruzuku Serikali kuu Sh. Bilion 7.4 na wahisani Sh. Bilion 3.6.
Hadi kufikia Disemba 2025 Sh. Bilion 5.8 zilipokelewa na kupelekwa kwenye utekelezaji wa miradi ambayo ni sawa na asilimia 46 ya bajeti ya maendeleo iliyoidhinishwa.
Katika utekelezaji huo Wilaya imekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kwenye sekta ya Elimu.
Wilayah ii ambayo ina shule za Msingi 114 kati ya hizo 92 ni za Serikali na 22 ni za binafsi na kwa upande wa Sekondari zipo Shule 36 (25 ni za Serikali na 11 zisizo za Serikali).
Aidha Sekta ya Elimu inaendelea kufanya vizuri ambapo Wilaya imeendelea kuhakikisha kuwa Wanafunzi wote wanapata fursa ya Elimu ikiwa ni utekelezaji wa Ibara ya 80 ya Ilani ya CCM
Mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya Elimu hadi sasa ni pamoja na ongezeko la Idadi ya Wanafunzi wa Shule za Awali na msingi kutoka 34,491 kwa mwaka 2024 hadi wanafunzi 34,847 kwa mwaka 2025 sawa na ongezeko la asilimia 1.
Vile vile kwa upande wa shule za Sekindari kidato cha kwanza hadi cha nne lipo ongezeko kutoka Wanafunzi 13,544 kwa mwaka 2024 hadi kufikia wanafunzi 14,348 mwaka 2025 sawa na ongezeko la asilimia 8.
Katika utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu elimu bila malipo Shule za Wilaya ya Kisarawe kwa kipindi cha Julai hadi Disemba 2025 zimepokea sh. Milion 858.2 ikiwa ni ruzuku ya uendeshaji wa shule za Msingi na Sh. Bilion 2.8 zilipokelewa kwa ajili ya ruzuku ya chakula, fidia ya ada na uendeshaji wa Shule za Sekondari.
Hali ya Ufaulu
Katika shule za Msingi kiwango cha ufaulu darasa la saba ni asilimia 85.65 na darasa la nne ni asilimia 92.8 kwa mwaka 2025.
Kadhalika kwa upande wa shule za Sekondari za Wilaya ya Kisarawe kiwango cha ufaulu Kidato cha sita ni asilimia 100, kidato cha nne asilimia 93.41 na kidato cha Pili asilimia 81.1 kwa Mwaka 2025.
Miundombinu ya Elimu ya Awali na Msingi
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe imepokea fedha za uboreshaji wa Miundombinu kutoka mapato ya ndani sh.69,745,438,438.29 kuwezesha ujenzi wa matundu 24 ya vyoo kupitia Mamlaka ya maji na Usafi wa Mazingira (SRWSS) katika shule za Kibasila na Chanzige B.
Pia kupitia mradi wa BOOST sh. Milion 474 zilipokelewa kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa 21 katika shule sita za msingi za Bwama, Mitengwe, Mloganzila B, Kiluvya A, Cholesamvula na Turini pia sh.Milion 100 za mradi huo zilipokelewa kwa ajili ya ukarabati wa vyumba nane vya madarasa shule ya Msingi Gwata.
Vilevile Sh. Milion 50 kutoka Serikali kuu zilipokelewa kwa ajili ya umaliziaji wa vyumba vitano vya madarasa katika shule za msingi za Kihare vyumba viwili vya madarasa, Kiluvya A vyumba viwili vya madarasa na Cholesamvula chumba kimoja.
Fedha za mapato ya ndani Sh. Milion 101 zilitolewa kuwezesha ukamilishaji wa nyumba ya mwalimu shule ya Msingi Kisangire, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Visegese na Mihugwe ujenzi wa matundu ya vyoo nane, yoo katika shule za Msingi za Titu na Mloganzila na ujenzi wa nyumba 1 ya mwalimu katika shule ya Msingi ya Kihare.
Mradi wa BOOST pia umewezesha ujenzi wa matundiu ya vyoo 48 katika shule za msingi sita za Bwama, Mitengwe, Mloganzila B, Kiluvya A, Cholesamvula na Turini kwa Sh. Milion 86.4 huku Sh. Milion 288.5 kutoka katika mradi huo zikipokelewa na kutumika kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Msingi Kibuta.
Mafanikio katika Miundombinu ya shule za Sekondari
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe imepokea fedha za uboreshaji wa Miundombinu kutoka katika mapato ya ndani Serikali kuu na wahisani.
Shilingi Milion 96.2 za mapato ya ndani zilipokelewa kwa ajili ya ukarabati wa maabara moja shule ya Sekondari Vikumburu, Sh. Milion 29, ukarabati wa maabara shule ya Sekondari Mfuru, Sh. Milion 23 ukamilishaji wa nyumba ya mwalimu ashule ya sekondari Kisarawe sambamba na ununuzi wa viti na meza katika shule ya Sekondari Mloganzila.
Kadhalika fedha kutoka Serikali kuu Sh.Miln 60 kwa ajili ukamilishaji wa maabara mbili za sayansi shule ya sekondari Kisangire na Sh. Milion 284 kupitia P4R kwa ajili ya ujenzi wa mabweni .
Sekta ya Afya
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe inamiliki Hospitali moja ya Serikali na vituo vya afya sita vinavyomilikiwa na Serikali na Zahanati 45 kati ya hizo za serikali 39.
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa kipindi cha Julai 2025 hadi mwezi Disemba imepokea Sh. Bilion 1.4 ikiwa ni fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu, wadau, wahisani mbalimbali pamoja na makusanyi ya ndani kwa ajili ya maboresho katika sekta ya afya.
Ununuzi wa Vifaa Tiba na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za sekta vimefanyika ili kuendelea kuboresha huduma za afya Wilayani.
Pia Halmashauri imepokea kiasi cha fedha kutoka Mfuko wa kupambana na Ukimwi, Kifua kikuu na Malaria Sh. Milion.57.5 likizo za watumishi na posho ya kujikimu ajira mpya shilingi Milion 40.
Katika kipindi cha Julai 2025 hadi Disemba 2025, Sekta ya afya imeendelea na usimamizi, ufuatiliaji na ukamilishaji wa miradi ambayo ilikuwa inatekelezwa katika kipindi cha 2024/2025 ambayo ni pamoja na ujenzi wa kituo cha afya Vikumburu, kituo cha afya Gwata na ukamilishaji wa ujenzi wa kituo cha afya Kiluvya .
Miradi mingine ni pamoja na ukamilishaji wa Zahanati ya Chang’ombe, zahanati ya Mafumbi, zahanati ya Bwama na kukamilisha zahanati ya Kitanga.
Katika kipindi chote hicho kwenye Halkmashauri ya Wilaya ya Kisarawe huduma bora za afya zimeendelea kuimarishwa kwenye jamii ikiwa ni pamoja na udhibiti wa magonjwa ya mlipuko ndani ya Wilaya.
Sekta ya Maendeleo ya Jamii
Wilaya ya Kisarawe inaendelea na utekelezaji wa Ibara ya 32(s) ya Ilani ya CCM kwa kutenga fedha kwa ajili ya mfuko wa Maendeleo ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu mujibu wa sheria kuwezesha makundi hayo kupata mikopo isiyo na riba.
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe inatekeleza kwa vitendo Sera ya Taifa ya maendeleo ya Uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kwa kuwawezesha Wanawake, Vijana na wenye ulemavu. Kushiriki katika shughuli za kiuchumi kwenye maeneo ya biashara, kilimo, ufugaji na usafirishaji.
Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri hiyo ilitenga sh. Milion 385.3 kwa ajili ya Mfuko wa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu na hadi kufikia mwezi Disemba 2025 Halmashauri kupitia mapato ya ndani imeshachangia sh. Milion 233.3 sawa na asilimia 60.56.
Kati ya fedha hizo Sh. Milion 93.3 zilikuwa kwa ajili ya Wanawake, kundi la Vijana Sh. Milion 93.3 na Watu wenye ulemavu Sh. Milion 46.6.
Kaatika kipindi cha Julai hadi Disemba 2025/2026 Halmashauri ilitoa mikopo ya jumla ya Sh. 110.6 kwa vikundi vitano vitatu vikiwa vya vijana ambavyo vilipatiwa sh. Milion 83 na viwili vya wanawake ambavyo vilipata Sh. Milion 27.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ilipokea Sh. Milion 102.2 kwa ajili ya shughuli za kuwalipa wanufaika wa kaya masikini pamoja na kufanya usimamizi na ufuatiliaji wa kaya hizo.
Katika kipindi cha kuanzia Julai 2025 hadi Disemba vikundi 13 vyq huduma ndogo za kifedha viliundwa na kusajiliwa na mpango umeweza kukaguliwa na wakaguzi wa nje (CAG).
Katika kipindi hicho pia biashara 463 za walengwa zilitembelewa na walipewa elimu ya namna ya kuziboresha ambapo ilipofika Septemba 30 sehemu ya pili ya mpango huo ilifika tamati.
Mafanikio katika sekta ya kilimo
Asilimia 95 ya wakazi wa Kisarawe ni wakulima wa mazao mbalimbali ya chakula na biashara, huku asilimia tano wakiwa ni wafanyabiashara na wafugaji.
Katika mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri kupitia kitengo cha Klimo, Mifugo na Uvuvi ilikisia na kupanga bajeti ya Sh. Bilion 2.1 na kati ya fedha hizo Sh. Bilion 1 ni fedha kutoka Serikali kuu, Miradi ya maendeleo sh. Milion 68.4, mapato ya ndani ya miradi ya maendeleo Sh. Milion 54 na mapato ya ndani matumizi ya kawaida na Sh. Milion 66.2 ruzuku ya matumizi mengine kutoka serikali kuu.
Kiwanda cha Kubangua Korosho
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe inatekeleza mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata korosho wenye thamani ya Sh. Bilion 2.9 lengo likiwa ni kuongeza thamani ya zao la korosho kwa kumuinua mkulima wa chini kiuchumi kwa kuuza mazao yake kiwandani moja kwa moja.
Halmashauri hiyo ipo kwenye taratibu za kutoa tangazo la kumtafuta mwekezaji wa kuendesha kiwanda ili Halmashauri inbaki na jukumu la kukusanya mapato ya mazao na majengo.
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa sasa imna viwanda 18, vikubwa vikiwa ni nane, vya kati vitano na na vidogo vitano ambavyo vimetoa zaidi ya ajira 741.
Aidha Halmashauri hiyo inaendelea kuhamasisha uwekezaji wa viwanda na tayuari imetenga eneo kubwa lenye hekari 1,100 katika kata ya Kazimzumbwi eneo ambalo linafaa kwa ujenzi wa viwanda vya aina zote.
Sekta ya ardhi
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ilipanga kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya Vijiji kuytoka ongezeko la Vijiji 45 kwa mwaka 2024/2025 hadi Vijiji 49kwa mwaka 2025/26 na kufikia Julai 2025 hadi Disemba tayari mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa Vijiji vine imeandaliwa na kukamilika ambavyo ni Gwata, Chang’ombe B, Kikwete na Mfuru.
Kadhalika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe katika kipindi cha mwaka wa fedha Julai 2025 hadi Disemba 2025 kupitia kitengo cha utamaduni imekusanya sh. Milion 10.8.
Kitengo hicho cha utamaduni pia kimefanikisha usajili wa kituo kimoja cha michezo ambacho kina malengo ya kutoa ajira kwa vijana ambao wana vipaji vya michezo.
Mapato ya Halmashauri
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kupitia vyanzo vyake vya vya mapato ya ndani ilikadiriwa kukusanya Sh. Bilion 5.8 na hadi kufikia Disemba 31 Halmashauri hiyo imekusanya Sh. Bilion 3.7 sawa na asilimia 65 ya bajeti ya mapato ya ndani iliyoidhinishwa.
Miradi ya Kimkakati inavyotekelezwa Kisarawe
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawekupitia idara ya utawala kilim, mifugo na uvuvi viwanda Biashara na Uwekezaji imeendelea kutelkkeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa jengo la utawala kupitia mapato ya ndani na fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu.
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe imetumia zaidi ya Milion 224 kwa ajili ya ujemnzi wa stendi ya daladala katika kitongoji cha Homboza kata ya Msimbu na Sh. Milion 98 kwa ajili ya viwanja 3027 na uidhinishaji wa viwanja 770 eneo la palalei kata ya Msimbu.
Pia Halmashauri hiyo imepokea Sh. Milion 700 kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la utawala na Sh. Milion 300 kwa ajili ya ununuzi wa samani za jengo hilo.
Mahitaji ya maji Kisarawe
Mahitaji ya maji kwa wakazi 52,046 walioko kwenye eneo linalohudumiwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Dar es Salam (DAWASA) katika Wilaya ya Kisarawe yanakadiriwa kuwa lita Milion 3.47 kwa siku mahitaji hayo yanakadiriwa kuongezeka hadi kufikia lita Milion 4.43 ifikapo kwama 2030.
Sehemu kubwa ya Kisarawe inapata huduma ya maji kutoka mtambo wa Ruvu juu wenye uwezo wa kuzalisha lita Milion 196 kwa siku ambapo katika wilaya hiyo yapo matenki matatu yenye ujazo wa lita Milion 6,315.
Sehemu kubwa ya wilaya hiyo katika kata ya Kisarawe na Kazimzumbwi zinahudumiwa na mtambo wa Ruvu juu kupitia mabomba yenye inchi 48 na 36.
Katika Wilaya ya Kisarawe upatikanaji wa huduma ya maji safi katika maeneo mengi inakadiriwa kufika wastani wa asilimia 80 kwa maeneo yanayohudumiwa na Dawasa Kisarawe.
Hata hivyo hadi kufikia Disemba 2025 Serikali imetekeleza na inaendelea kutekeleza miradi yenye thamani y ash. Bilion 36.4 katika Wilaya ya Kisarawe n ash. Bilion 2.6 zimegharamia miradi ya maji safi ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Wananchi 4,3477 wananufaika na miradi ya maji safi iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa ambayo imeongeza upatikanaji wa maji safi kupanua mtandao wa usambazaji na kuboresha miundombinu ya usafi wa mazingira.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED