Wilaya ya Rufiji kupitia Halmashauri, na taasisi nyingine za Serikali inaendelea na utekelezaji wa shughuli za maendeleo kama zilivyoelekezwa katika Ilani ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Shughuli nyingi zimetekelezwa na kukamilika na zingine zinaendelea kutekelezwa na zipo hatua mbalimbali za ukamilishaji.
Wilaya ya Rufiji inaendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika kulinda raia na mali zao kwa kuwashirikisha Wananchi katika ulinzi wa mali na jamii zao.
Pia inaendelea na mikakati yake ya kuzuia rushwa na kuchukua hatua kali za kisheria kwa wote wanaothibitika kujihusisha na vitendo vya rushwa na uvunjifu wa maadili kwa kuwahusisha na kuwashirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo.
Kadhalika kipaumbele cha kuimarisha huduma za Serikali kwa kuhakikisha huduma zinapatikana mapema, kwa ufanisi na karibu na Wananchi kinaendelea sambamba na kuimarisha uwajibikaji miongoni mwa Viongozi na Watumishi wa Umma.
Ibara ya 33 (e) ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025/2030, inaelekeza kuwa na sera madhubuti za uchumi jumla ili kupunguza utegemezi wa kibajeti kwa kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani, ikiwemo kuibua vyanzo vipya vya mapato na kuongeza idadi ya walipa kodi, kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara na kukusanya maduhuli yote kwa kutumia mifumo ya kielektroniki.
Wilaya ya Rufiji, imeendelea kusimamia Halmashauri katika Uimarishaji wa Ukusanyaji wa Mapato kwa kuongeza vyanzo Vipya vya mapato, matumizi ya mifumo ya kielektroniki na kupanua wigo wa walipa kodi.
Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Rufiji anavyojivunia ukusanyaji wa mapato
Katika kipindi hiki cha kuanzia Mwezi Julai, 2025 hadi Juni, 2026 Halmashauri imeweza kukusanya Sh.Bilion 6.3 sawa na asilimia 93.2 ya lengo la Mwaka wa fedha 2025/26 la kiasi cha shilingi 6.7.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Rufiji Simon Berege anasema katika Mwaka wa fedha 2025/26 Halmashauri ilipanga kupokea na kutumia kiasi cha Sh.Bilion 36 kwa ajili ya kutekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo.
Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Juni, 2026 kiasi cha Shilingi Bilion 26.6 zimepokelewa, sawa na asilimia 74 ya bajeti ya Halmashauri.
Berege anasema, “Halmashauri hiyo imeendelea kusimamia utekelezaji wa shughuli na miradi ya maendeleo ili kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora na kuondoa kero mbalimbali.”
Uwezeshaji wananchi kiuchumi
Anasema Ibara ya 33 (a - g) ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025/30, inaagiza kutoa msukumo katika Kuongeza fursa za ajira kwa Vijana, kuongeza kipato kwa Wananchi na kupunguza umaskini.
Mkurugenzi huyo anaeleza kwamba katika kipindi cha Januari Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Rufiji hadi Juni, 2026 Wilaya ya Rufiji imefanikiwa kutoa Mikopo yenye thamani ya sh. Bilion 1.2 kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu.
Anafafanua kwamba kiasi cha Sh.Milion 44,079,000 ni fedha za bakaa, na Sh. Milion 184,251,048 ni fedha za asilimia kumi 10 za mapato ya ndani na kiasi cha sh.Bilion 1 ni fedha za marejesho.
Mikopo hiyo imetolewa kwa Vikundi 121, kwa ikiwa ni pamoja na vikundi 63 vya Wanawake, vikundi 47 vya Vijana na vikundi 11 vya Watu Wenye Ulemavu.
Aidha, hadi kufikia mwezi Juni, 2026 Halmashauri katika mapato yake ya ndani (bila vyanzo lindwa) imechangia kwa asilimia 63 kwenye mfuko wa maendeleo ya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu sawa na sh. Milion 189.2.
Utoaji Mikopo kwa Mwaka wa Fedha (Januari hadi Juni, 2026)
Anasema kuwa mikopo hiyo imeendelea kuwa chachu ya kuleta maendeleo (mafanikio) kwa Wajasiriamali ikiwa ni pamoja na kuondoa utegemezi mkubwa katika familia hasa akina Mama waliokuwa wanawategemea waume zao.
Mafanikio mengine ya mikopo hiyo yamepatikana kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi yenye mlengo wa viwanda kama vile usindikaji wa nafaka, ushonaji n a mvinyo ambapo Vijana wengi wamekuwa mwamko katika kushiriki shughuli za kiuchumi na kupunguza wimbi la vijana wasiokuwa na kazi kurandaranda mitaani.

Aidha, uhamasishaji umeendelea kufanyika kwa Wananchi kujiunga katika vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kujisajili na kufungua akaunti, ambapo Wananchi 623 Wanaume wakiwa ni 223 na wanawake 400.
Rufiji inajivunia utekelezaji wa mpango wa TASAF. K a t i k a kipindi hiki cha Januari hadi Juni, 2026 mpango wa Taifa wa kutoa bima ya afya kwa wote (NHIF) kupitia programu ya TASAF umetekelezwa katika awamu mbili na awamu ya kwanza umetekelezwa mwezi Februari 11 mwaka huu katika kata tano ambazo ni Utete, Ikwiriri, Umwe, Mgomba pamoja na Mohoro/ Shela (Mohoro Magharibi na Mashariki na Kijiji cha shela).
Utekelezaji wa mpango huo wa kutoa bima ya afya kwa awamu ya pili ulitekelezwa kuanzia Februari 2026 hadi katika kata nane ambazo Walengwa waliosajiliwa katika mfumo wa Bima ya Afya kwa wote na kata hizo Mohoro/ Shela, Chumbi, Mbwara, Chemchem, Mkongo, Ngorong na Mwaseni.
Sekta ya Kilimo,Mifugo na Ushirika
Sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi, na ushirika imeendelea na kazi ya usimamizi, na ufuatiliaji wa shughuli za kilimo, mifugo na ushirika ambapo katika kipindi hiki cha Januari hadi Juni, 2026 Wilaya imefanya usimamizi wa shughuli mbalimbali ikiwemo ya uendelezaji wa zao la Korosho.
Katika kipidi hicho, sekta ya kilimo imeendelea kutoa huduma ya ugani kwa kuhimiza Wakulima kufanya palizi katika mashamba ya Korosho, sambamba na kutoa elimu kuhusiana na upandaji wa mikorosho mipya.
Aidha, Wilaya imepokea kilo 9,935 za mbegu bora ya korosho kutoka Bodi ya Korosho Tanzania na kufanikisha kuzalisha miche bora 1,174,725 kupitia vikundi 57 vya Wanawake na Vijana, ambayo imegawiwa bure kwa Wakulima walioandaa mashamba kwa ajili ya kupanda.
Pia umefanyika uendelezaji wa kilimo cha zao la Pamba .
Katika msimu wa mwaka 2025/26 sekta ya kilimo kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba imeendelea kufanya uhamasishaji wa upandaji wa zao la pamba kwa msimu wa masika na tayari kata 9 zimefikiwa.
Aidha shughuli za upandaji wa zao la pamba na usambazaji wa viuatilifu vya kudhibiti wadudu na magonjwa linaendelea.
Uendelezaji wa Sekta ya Ushirika
Sekta ya Ushirika imeendelea kutekeleza mambo utoaji wa elimu na mafunzo ya usimamizi wa vyama vya Ushirika (AMCOS 18), kwa wajumbe wa bodi 110, na Wanachama wa vyama hivyo 376 vilivyopo Rufiji.
Vilevile usimamizi na utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa vyama vya Ushirika (MUVU) katika vyama vya Ushirika vya mazao na masoko umeendelea huku elimu na mafunzo ya uwekezaji, haki na wajibu wa wanachama na jinsi ya kuongeza thamani zao la korosho kupitia ubanguaji, yakitolewa kwa AMCOS 16 na Wanachama 342.
Sekta ya Elimu
Msingi Katika kipindi cha Januari hadi Juni, 2026 Juni, 2026, jumla ya Wajasiriamali/ Wamachinga 40 kati yao Wanaume 29 Wilaya ya Rufiji imefanikiwa katika maeneo uandikishaji wa Wanafunzi wa darasa la awali kwa asilimia 84.4, darasa la kwanza asilimia 108.5 sambamba na wanafunzi 15 wa darasa la MEMKWA.
Katika kipindi hicho pia hali ya afya na lishe kwa Wanafunzi katika Shule zote 60 za Msingi inaridhisha, ambapo kati ya wanafunzi 35,506, wanafunzi 14,463 sawa na asilimia 43.24 wanapata chakula cha mchana shuleni.
Vilevile Wilaya ya Rufiji imeendelea na ujenzi wa miundombinu muhimu kwa ajili ya maendeleo ya elimu ya msingi ambapo Sh.Bilion 6.6 fedha za mapato ya ndani na Serikali Kuu, zimetumika katika ujenzi wa Shule mpya 03, ukarabati na ujenzi wa vyumba vya madarasa 56, nyumba za walimu 149, na matundu 204 ya vyoo, ambapo nyumba 134, vyumba 37 vya madarasa na matundu yote 194 yamekamilika na yanatumika.
Aidha, kiasi cha Sh. Milion 336.6 zimetumika katika utoaji wa elimu bila malipo, ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Azimio Sh. Milion 386.5,ujenzi wa Shule mpya ya Elimu ya Awali na Msingi ya Mkondo mmoja Ikwiriri sh. Milion 291.5 na ukarabati wa vyumba vine vya madarasa, nyumba tatu za walimu na ofisi mbili za walimu.
Shughuli nyingine zilizofanyika ni ujenzi wa matundu sita ya vyoo, vyumba vya madarasa viwili na matundu sita ya vyoo Shule ya Msingi chumbi, ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa, nyumba 4 za mwalimu na ofisi Shule ya msingi Katundu.
Utekelezaji katika Sekta ya Elimu Sekondari
Katika Sekta hii ya Elimu Sekondari Sh. Bilion 2 zimetumika katika ujenzi na ukamilishaji wa vyumba vya madarasa 16 na matundu 36 ya vyoo,sambamba na ukamilishaji wa vyumba sita vya maabara, na mabweni 12.
Hadi kufikia mwezi Juni, 2026 jumla ya vyumba vya madarasa 10, maabara 03, mabweni 06, meza na viti 683 na matundu 26 ya vyoo yamekamilika na yanatumika.
Aidha, shilingi Bilioni 1.2 zimetumika katika utoaji wa elimu bila malipo.
Sekta ya Afya
Katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni, 2026 Sekta ya afya imefanikiwa kutekeleza shughuli zake kwa ufanisi ikiwemo huduma ya dawa, vifaa tiba na Vitendanishi.
Wilaya ya Rufiji ina jumla ya Vituo 41 vya kutolea huduma za afya (Hospitali 1, Zahanati 35 na Vituo vya afya 5) ambapo vya binafsi ni 4, na vya Serikali ni 37.
Aidha, vituo hivyo, vina usajili Bohari ya Dawa (MSD) na vinavyopata ruzuku ya Serikali. Upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa kipindi cha Januari- Juni, 2026 ni kwa asilimia 86.98.
Vile vile katika kipindi hicho cha miezi sita usambazaji wa chanjo na vifaa vyake kwa vituo vyote 35 vinavyotoa huduma ya chanjo kila mwezi umefanyika kwa asilimia 100. Vituo vimefanikiwa kufanya huduma Mkoba sehemu ambazo hazifikiki kwa lengo la kuhakikisha Watoto wote wanapatiwa chanjo na kwa kipindi hii huduma mkoba zilizopangwa kufanyika ni 190 na zilizofanyika ni 137 sawa na 72%.
Huduma ya Mama na Mtoto zimeendelea kutolewa katika vituo 32 vinavyotoa huduma za kujifungua na vituo 34 vinavyotoa huduma za RCH kati ya vituo 38.
Wajawazito 888 kati ya 1,937 sawa na asilimia 51.2 walihudhuria kilini mapema kabla ya wiki 12 wakati wajawazito 1,928 kati ya 1,967 sawa na asilimia 98 wakijifungulia kwenye kituo cha huduma.
Kadhalika ugawaji wa vyandarua ambapo umefanyika katika kipindi hicho ambapo jumla ya vyandarua 4,139 viligawiwa kwa Wananchi wakiwemo wazee wa miaka 60 na zaidi waliofika vituoni kupata matibabu ambao ni 435, Watoto 56 chini ya maika 5 waliolazwa vituoni na kutibiwa malaria kali.
Wengine walionufaika na vyandarua hivyo ni wateja wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI waliohudhuria katika vitengo vya maisha zaidi [CTC] vituoni ni 185.
Pia Wajawazito waliohudhuria kliniki vituoni wenye hudhurio la kwanz 1,892 sawa na asilimia 98 pamoja na watoto waliohudhuria kliniki kupata chanjo ya kwanza ya Surua Rubella na kupewa vyandarua ni 1,571 ni sawa na asilimia 100.
Sekta ya Afya, Wilaya inaendelea na uboreshaji wa miundombinu a m b a p o kwa kipindi cha kuelekea mwi shon i mwa mwezi Juni, 2026, Halmashauri inaendelea kutekeleza ujenzi ya mi radi ya sekta y eny e jumla ya kiasi cha Sh. Bilioni 4 zimetumika.
Fedha hizo zimetumika katika ujenzi na ukamilishaji wa nyumba tatu za Watumishi, Zahanati sita, Vituo vitano vya afya, na ujenzi wa miundombinu ya Hospitali ya Wilaya (Jengo la Watoto Njiti, Maabara, Jengo la Kufulia), miundombinu hiyo, utekelezaji wake unaendelea.
Sekta ya Ardhi
Katika kipindi cha Januari hadi Juni, 2026, Wilaya ya Rufiji imesimamia na kutekeleza shughuli mbalimbali ikiwemo ya wataam wa Wilaya kutoa ufafanuzi na ushauri mbalimbali kuhusu masuala ya ardhi katika Kata sita za Ikwiriri, Mgomba, Umwe, Mohoro, Mwaseni, Chumbi na Mbwara.
Tayari Halmashauri imekamilisha upimaji wa viwanja 113 katika maeneo mbalimbali ya Mji ambapo viwanja 109 vipo Mgomba , kiwanja 1 kipo Mloka, viwanja 3 vipo Ikwiriri. Viwanja hivi ni kutokana na maombi binafsi ya Wananchi.
Halmashauri pia inaendelea na usimamizi wa mauzo ya viwanja vya mradi wa Halmashauri katika Kitongoji cha Nyandumbi uzaji wa viwanja kwa njia ya mfumo wa TAUSI bado unaendelea.
Hati miliki 39 za kisheria zimeandaliwa na kuwasilishwa kwa Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kusainiwa na kusajiliwa. Pia, hati miliki 21 za Kimila zimeandaliwa na kusajiliwa.
Wilaya imefanya uthamini wa awamu ya tatu eneo la Nyamwage kwa ajili uwekezaji wa kilimo cha ndizi na kazi bado inaendelea huku uthamini katika Kijiji cha Chumbi C kwenye eneo linalotarajiwa kufanyika uwekezaji wa kilimo cha zao la Chikichi ukiendelea .
Sekta ya Miundombinu
Wilaya ya Rufiji ina mtandao wa barabara wenye jumla ya Kilomita 523.51, ambapo Km 431.089 sawa na asilimia 82.3 ni za udongo, Km 78.14 sawa na 14.9 ni kiwango cha changarawe, na Km 14.281 ni za kiwango cha Lami.
Kwa mwaka huu wa fedha 2025/26, TARURA Wilaya ya Rufiji inatekeleza shughuli mbalimbali za Ujenzi na ukarabati wa barabara kwa bajeti iliyopangwa.
Katika Sekta hiyo, Wilaya kupitia TARURA Imeendelea na uboreshaji wa miundombinu ya barabara, ambapo katika kipindi cha kuishia Mwezi Juni, 2026, Wilaya inatekeleza mi radi yenye jumla y a sh.Bilion 30.6 na ipo hatua mbalimbali za utekelezaji.
Upo ujenzi wa barabara za Lami mji wa Ikwiriri km 20 ujenzi wa barabara za lami mji wa Ikwiriri Mjini uanatekelezwa na wakandarasi M/s Afritrust Group Limited, M/s Morcep Investment Company Limited na M/s Trinity Manufacturering Services jumla ya kilometa 7.5 ambao mradi una gharama ya Tsh. 5,878,473,352.00 .
Ujenzi wa Daraja la Mohoro M 120 ambao unatekelezwa Mkandarasi MAC Contractors Co. Ltd kwa gharama ya Shilingi 17.85 bilioni.
Sekta ya Maji.
Wilaya ya Rufiji kwa kushirikiana na Wadau wa maendeleo imeendelea kujenga Miradi ya Maji ili kufikia lengo la Kitaifa la upatikanaji wa huduma ya Maji safi na salama ndani ya mita 400 kwa asilimia 85 Vijijini na asilimia 90 Mijini ifikapo 2030.
Mahitaji ya Maji katika Wilaya Rufiji ni lita 3,580,475 kwa siku ambapo kwa sasa idadi ya Wananchi wanaopata huduma ya Maji safi na salama ni asilimia 92.
Katika mwaka wa fedha 2025/26, Wilaya inatekeleza Miradi ya Maji na usafi wa Mazingira yenye thamani ya shilingi 699,498,637.68 ambayo itanufaisha Jumla ya Wananchi 35,591 katika Kata za Mwaseni, Mkongo na Shela.
Wilaya pia kupitia RUWASA Imeendelea na uboreshaji wa miundombinu ya Maji, ambapo miradi yenye thamani ya Sh. 699,498,637.68 ipo hatua mbalimbali za utekelezaji.
Sekta ya Nishati
Hali ya Upatikanaji wa Umeme katika Wilaya ya Rufiji ni kwa kata zote na pia katika Vijiji 30 vyote vina umeme.
Wilaya ya Rufiji baada ya kupandishwa hadhi na kuwa Halmashauri ya Mji, ina mitaa 36 na mitaa hiyo yote nayo ina umeme tayari na katika Vitongoji 99, tayari 68 vina umeme mpaka sasa na kubakiwa na vitongoji 31 pekee.
Aidha, Wakala wa umeme vijijini (REA) wamepata Mkandarasi atakayetekeleza mradi huo wa kukamilisha vitongoji vyote vilivyobaki katika Wilaya ya Rufiji ndani ya mwaka wa fedha ujao 2026/27.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED