KARIBU tena msomaji wangu kwenye safu hii pendwa ya Maisha Ndivyo Yalivyo. Hapa utajifunza na kusikia vituko mbalimbali vinavyotokea kwe nye maisha yetu ya kila siku. Wiki iliyopita tuliona ndoa za mapema kwa vijana wetu zinavyosambaratika uda mfupi baada ya kuoana. Je, ni kwa sababu hawakufundwa vema kabla ya kuingia kwenye mkataba wa ndoa?
Sababu ni nyingi zinazochang ia hali hiyo.Leo tujadili baadhi ya wakwe wanavyosababisha mitafaruku ya mapema katika ndoa changa. Dada mmoja alifunga ndoa miaka mitatu iliyopita na kuba hatika kupata mtoto mmoja. Lakini sasa anaiona ndoa chungu kutokana na vituko vya mama mkwe wake.
Anasema, mama mkwe tangu niolewe na kijana wake hodi haziishi nyumbani kwangu. au hawafundishwi kabla ya kuin gia kwenye ndoa. Nalo ni uhusi ano kati ya mke na mama mkwe.
Kila mwanamke ana umuhimu ndani ya jamii, haijalishi ni mzee, kijana, tajiri au masikini. Tena akiamua anapiga kambi hadi wiki moja. Na ndani ya muda huo, ni fujo hanipi utu livu.Atakuwa mdadisi, ataniam risha nifanye hiki na kile kama vile zitambui wajibu wangu kwenye nyumba yangu. Ha nipi uhuru wa kuamua jambo.
Wakati mwingine ataingia jikoni na kupika huku akinisimanga si jui kupika, hali inayonikosesha raha sana. Mume wangu nampenda sana lakini mama yake mzazi anani katisha tamaa. Wakati mwingine anan igombeza bila sababu ya msingi. Nawaza sana kama vile nimein gia nyumba ambayo siyo sahihi! Sijui nifanyeje, niko njia panda.
Nikimsimulia mume wangu vituko hivi ni kama vile haniami ni au hanielewi. Upo wakati an amtetea badala ya kuwa upande wangu. Natamani hata kuikim bia ndoa hii! Hivyo ndivyo ana vyosimulia dada huyu. Kuna jambo moja muhimu ambalo vijana wengi hawaelewi Mwanamke yoyote anaweza kuwa mke mzuri, mama mzuri, mama mkwe mzuri au mama mkwe mwenye kipawa.
Hebu sasa tuone mama mkwe ni nani. Huyu ni mama mzazi wa mume wako. Mama mkwe anaweza kuwa mzuri na mwenye kujenga. Anaweza kuwa nguzo ya ku shikilia na kufundisha familia changa. Ni mzoefu katika masuala ya ndoa, na kwa miaka yake ya uzoefu katika mambo ya ndoa, anaweza kuwa chanzo cha hek ima kwa wake wachanga ambao bado wanajifunza mambo mbal imbali katika ndoa zao.
Mama mkwe anamfahamu vizuri mtoto wake wa kiume na ana jua vema jinsi ya kumhudumia/ kumtunza. Hata kama ameoa, mama yake anamtegemea ka tika mahitaji mengi. Kadhalika, kama kulivyo na mama wake wema, wapo wa naopenda kujiinua na hawashi kiki/hawavumiliki. Wao huona mke wa mtoto wao kama adui, na kwamba huyo mke anahitaji kuchunguzwa kwa kila kitu ana chokifanya.
Kwa hiyo, hufanya juu chini kuhakikisha huyo mke wa mtoto wao anaishi maisha magumu ili ashindwe kufanikiwa katika ndoa yake.Wao huona nyumba ya mtoto wao ni kama nyumba yao ya pili, hivyo hutaka kuita wala. Mara nyingi wake hujikuta wanaanguka chini ya miguu ya hawa mama wakwe! Ni ukweli usiopingika kuwa wanawake wengi wamepoteza ndoa kwa sababu ya hawa wak we.
Kama siyo kupoteza ndoa, wengi wamejikuta wakichukua nafasi ya “mke wa pili” ndani ya nyumba zao. Kwa nini? Ni kwa sababu mama wakwe wengi hupenda kujiinua na kuchukua majuku mu ndani ya nyumba za watoto wao wa kiume kama “wake wa kwanza”. Msomaji, yapo mambo mengi yanahitaji kujadiliwa na ku fundishwa kuhusu uhusiano kati ya mke na mama mkwe.
Lakini kwa bahati mbaya, wengi hawalichukulii suala hili kwa uzito. Katika tamaduni za Afrika, ni muhimu sana kuonge lea suala hili la mama mkwe tu napokuwa tunajadili ndoa. Hii ni kwa sababu wao wanahusika kwa sehemu kubwa kujenga au kubomoa ndoa za watoto wao. Mfano, kama mama mkwe anampenda mke wa mtoto wa kiume, itakuwa ni vigumu sana kwa huyo kijana kumpa talaka huyu mwanamke hata kama amekosea.
Lakini kama mama mkwe na ndugu wa mwanaume ha wampendi huyo mwanamke, ni Mungu pekee ndiye atakayereje sha hiyo ndoa. Kwa maana mkwe na ndugu za mwanaume watahakikisha wanampa wakati mgumu, lengo likiwa atoke kwa mume wake! Mwanamke mwenye akili ata jitahidi kumpenda mume na kuhudumia nduguzake vizuri.
Ujumbe 0715268581.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED