Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro ameridhishwa na ushirikishwaji wa vijana katika uendelezaji wa miradi ya gesi asilia inayoendelea mkoani Mtwara.
Akizungumza katika banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli kwenye maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam(DITF), Kamanda Muliro amesema ni vema miradi hiyo ikaendelea kushirikisha vijana kwani serikali inaendelea kutoa hamasa kwa kundi hilo kujikita katika sekta ndogo ya mafuta na gesi.
Kwa upande wake Mjiolojia kutoka PURA Lukelo Matimbwi amemueleza Kamanda Muliro kuwa katika mradi wa uzalishaji wa gesi asilia unaoendelea Mnazi Bay zaidi ya asilimia 90 wanaofanya kazi hapo ni vijana wa kitanzania.
Ameongeza kuwa katika mradi wa uzalishaji wa gesi asilia Songo Songo pia ushirikishwaji wa vijana wa Kitanzania ni mkubwa katika utekelezaji wa mradi huo.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED