Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi ameonya wanaopanga kuandamana.
Amewaomba wazazi 'kuwakanye' watoto wao kuingia kwenye mkumbo wa ushawishi kwenye maandamano, akisisitiza kwamba wamejipanga kila mahali kuwakabili watakaojaribu kuandamana au kuvunja kuvunja amani ya nchi.
"Niwaombe wazazi, wawakanye watoto wao, wasiingie mkumbo na kujaribu kuvunja amani ya nchi
mkanyemwanao, mwambie jinai hailipi na bahati mbaya jinai haiozi.utafanya leo utakimbia nje ya nchi lakini haiozi, tutakumata tu."
Ametoa kauli hiyo leo alipotembelea maonesho 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF).
"Tumejipanga kila maeneo na tunaendelea kujipanga, niwahakikishie Watanzania kwamba hakuna tushio lolote la usalama litakaokuwapo,"amesema Katambi.
"Halafu serikali haipangiwi tarehe, hakuna aliye juu ya sheria, tutaendelea kuchukua hatua kwa mharifu yeyot, kwa mtu ambaye atatishia au kufanya kitu chochote cha uharilfu tutamkamata.Na tumejipanga kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama ili kuhakikisha raia anayepaswa kwenda kwenye shughuli za kiuchumi aende na anaeenda shule aende."
Kadhalika, Katambi amesema kwa siyo Tanzania siyo salama kwa waharifu.
"Niwaambie tu kwamba, kwa sasa Tanzania si salama kwa waharifu wa aina yoyote, Tanzania tuliyoachiwa itaendelea kuwa salama na tutailinda."
"Utaratibu wa maandamano na mikusanyiko yote imetajwakwenye sheria zetu, sasa wasizitumie vibaya kwa kuwa eti tumekuwa tukiwavumilia."
Amewaonya pia wale wote wanaorusha maudhui ya kuvunja amani kwenye mitandao.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED