Makamu wa Rais, Balozi Dk. Emmanueli Nchimbi amesema serikali ina mpango wa kuboresha zaidi maonesho ya Biashara ya Kimatafaya Dar es Salaam(DITF), ifikapo mwaka 2050.
Amesema maboresho wanayotarajia kufanya ni kuyaweka maonesho hayo yasiwe tu mahala pa kuonyesha biashara pekee, bali kitovu cha ubunifu, utafiti, teknolojia na biashara za kimataifa pamoja na kuunganisha wawekezaji na wabunifu.
Dk. Nchimbi amesema hayo juzi Dar es salaam katika usiku wa tuzo za dhababu zaa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Nchini (TANTRADE), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 ya DITF.
Pia, amesema wanataka maonesho hayo yawe ni sehemu itakapotumika kuzindua biashara mpya za Tanzania kwa soko la dunia na ukuaji wa biashara wa Tanzania na Afrika.
Amesema miongoni mwa mambo ambayo serikali inasisitiza ni eneo la utafiti, ubunifu na matumizi ya akili bandia biashara, teknolojia na mifumo ya kisasa ili viwe ni nguzo ya uchumi wa Tanzania.
Dk. Nchimbi amesema imedhamiria kujenga uchumi shindani wa viwanda ili kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kipato cha kati cha juu, huku kwa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.
“Na matokeo ya haya, tutashuhudia matokeo ongezeko la viwanda vinavyoendelea kujengwa, uzalishaji ukiongezeka, ajira zikiongezeka na bidhaa za Tanzania zikiendelea kupata nafasi kubwa zaidi katika masoko ya kimataifa,” alisema Dk.Nchimbi.
Ametoa wito kwa wazalishaji wote kutumia alama ya biashara ya Tanzania ‘Made ina Tanzania’ ili kujenga hadhi ya biashara za nchini na kuongeza ushindani wake katika soko la dunia.
“Tunataka kujenga alama ya biashara ya Tanzania, ambayo si biashara pekee, bali ni heshima ya taifa kwa kuonesha ubora wa bidhaa, hivyo ni vema tuitumie.”
Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, serikali imejipanga kuuza bidhaa zilizoongezwa thamani katika miaka 50 ijayo, ikiwa ni mkakati wa kujiimarisha katika biashara ya kimataifa kwa kuuza bidhaa zilizokamilika, zenye chapa zenye nguvu, teknolojia, ubunifu na maarifa.
Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Dk Latifa Mohamed Khamis amesema maonesho ya DITF yamezalisha fursa za biashara na uwekezaji zenye thamani ya takribani Sh. trilioni 129.231 katika kipindi cha miaka 50.
Amesema DITF imeiweka Tanzania katika ramani ya biashara ya kimataifa na kwamba maadhimisho ya miaka 50 ya maonesho hayo ni ya kutambua na kuthamini mchango wa wadau wa biashara na uwekezaji.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED