Uchumi wa dunia, vita ya Iran ajenga za G7

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:19 PM Jun 16 2026
Uchumi wa dunia, vita  ya Iran ajenga za G7
Picha:Mtandao
Uchumi wa dunia, vita ya Iran ajenga za G7

Viongozi wa nchi wanachama wa kundi la mataifa saba yenye nguvu za kiuchumi duniani (G7), unaanza rasmi hivi leo katika mji wa mapumziko wa Ufaransa wa Evian-les-Bains, huko Ufaransa.

Viongozi hao watajadili kuhusu migogoro ya Iran na vita vinavyoendelea nchini Ukraine. 

Mkutano huo unafanyika saa chache baada ya Marekani na Iran kufikia mpango wa makubaliano ya kumaliza vita vya Mashariki ya Kati vilivyodumu kwa zaidi ya miezi mitatu, huku mashambulizi yakiongezeka kati ya Urusi na Ukraine.

Viongozi hao wa G7 watajadili pia masuala ya uchumi wa dunia na kujaribu kuimarisha uhusiano wao na Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye mara kadhaa amewakosoa washirika wake kwa kutumia fursa za Marekani katika biashara, lakini wakashindwa kuisaidia Marekani pale inapohitaji msaada hasa wakati wa vita vya hivi karibuni kati yake na Iran.

Kundi la G7 linaundwa na nchi saba zilizoendelea zaidi Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza na Marekani.

Nchi hizo zinaongoza kwa utajiri wa kitaifa, zikiwa na asilimia 64 ya utajiri wote duniani takribani Dola za Marekani trilioni 263 kwa makadirio yam waka 2014.
DW