Baadhi ya wawekezaji katika sekta ya mafuta na gesi asilia, wameendelea kujitokeza kwenye banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli kwenye maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF),kuangalia fursa za kuwekeza katika sekta hiyo.
Miongoni mwa waliofika katika banda hilo ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Octant Energy, Richard Schmitt, ambaye amesema yuko tayari kuwekeza zaidi katika sekta hiyo hapa nchini.
Tayari Octant Energy ni miongoni mwa wawekezaji katika sekta hiyo ya mafuta na gesi hapa nchini ambao wameonesha nia ya kuongeza zaidi uwekezaji katika eneo hilo.
Amesema wanavutiwa kuendelea kuwekeza Tanzania kwa sababu ya mifumo wezeshi ya uwekezaji iliyowekwa na kwamba wako tayari kuongeza uwekezaji huo kwa kuzingatia sheria zilizowekwa na nchi.
Schmitt amesema kampuni hiyo inaendelea kutekeleza shughuli zake za uwekezaji kwa kushirikiana kwa karibu na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli na wadau mbalimbali waliopo kwenye sekta hiyo.
Akiwa katika banda la Mamlaka hiyo, Schmitt amepata elimu kuhusu mfumo wa usimamizi wa shughuli za utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini pamoja na rasili Petroli zinazoendelezwa kwa kuzingatia sheria na uwazi.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED