Kushuka bei za mafuta kulete nafuu kwa mwananchi wa kawaida

By Mhariri Mtendaji , Nipashe
Published at 06:42 PM Jun 18 2026
 Kushuka bei za mafuta kulete nafuu kwa mwananchi wa kawaida
Picha: Mtandao
Kushuka bei za mafuta kulete nafuu kwa mwananchi wa kawaida

KWA miezi kadhaa kumekuwa na kilio kuhusu kupaa kwa bei za mafuta. Sababu kubwa ya ku panda huko kwa bei za mafuta imekuwa ikielezwa kuwa ni vita kati ya Marekani na Iran huko Mashariki ya Kati. Kilio cha kupanda kwa bei za mafuta ambazo kwa Tan zania zimekuwa zikitangazwa kila mwezi, kimesababisha ongezeko la gharama za maisha kwa watu wa ngazi zote.

Watu wa kawaida, kwa mfano, wa naumia kutokana na kupanda kwa bei za vyakula na bidhaa wanazotumia kila siku. Wazalishaji viwandani pia wa nalazimika kupandisha bei za bidhaa kutokana na gharama za uendeshaji kama vile nishati wanayotumia pamoja na uagi zaji wa malighafi na vipuri ku toka ndani na nje ya nchi.

Vipuri, malighafi pamoja na baadhi ya vyakula vinaagizwa kutoka nje ama kutokana na uwezo mdogo wa uzalishaji wa ndani au kutokutengenezwa kabisa. Kwa jumla, kupaa kwa bei za mafuta kumesababisha athari kubwa katika kila sekta na jamii kwa ujumla, hata bei za bid haa hazishikiki kwa sababu ya mafuta, sababu kubwa ambayo imeku wa ikitajwa kuchangia ongeze ko hilo ni vita baina ya mataifa hayo mawili. 

Bei ya kitoweo, kwa maana ya nyama na samaki katika Jiji la Dar es Salaam, kwa mfano, iko juu tangu kuanza kwa vita hivyo kwa sababu ya gharama za usafirishaji kutoka mikoani wanakotolewa ng’ombe na sa maki. Hata mboga za majani ambazo ni tegemeo la wengi zimepun guzwa kiwango, sababu kubwa ikidaiwa kuwa ni ongezeko la bei za mafuta. 

Hata hivyo, kuna habari njema za kusitishwa kwa vita vya Iran vinavyohusisha Marekani na mshirika wake Israel dhidi ya Iran kwamba kutasababisha ahueni ya bei ya mafuta hali ita kayosababisha kupungua kwa makali ya maisha ya kila siku. 

Matokeo ya kusitishwa kwa mzozo huo yameanza kuone kana baada ya kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia. Bei za mafuta katika soko la dunia zimeshuka kwa takribani silimia 5.5, baada ya Marekani kusema pande husika zimefikia makubaliano ya kumaliza vita kutokana na mkataba utakaoti wa saini keshokutwa. 

Kwa mujibu wa vyanzo mbal imbali vya kimataifa, bei hizo za mafuta zilishuka kwa viwango vya chini zaidi, huku masoko yakitathmini uwezekano wa kurudi kwa usambazaji kupi tia Mlango-Bahari wa Hor muz baada ya kupitishwa kwa mpango wa awali wa kumaliza vita.  Takwimu za soko la dunia zinabainisha kuwa mikataba ya mafuta ya Brent ya siku zijazo imepungua hadi dola 81.00 (Sh. 212,653) kutoka dola 107 (Sh. 280,912) kwa pipa, ikielezwa kuwa ni kiwango cha chini zaidi kushuka tangu Machi 4, mwaka huu. 

Kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia ni dhahiri kwamba kutaleta nafuu kwa nchi kwa maana ya watumiaji wa kawaida wa nishati hiyo pamoja na wazalishaji mali vi wandani na wasafirishaji. Pamoja na ahueni hiyo kwa watumiaji wakiwamo wami liki wa vyombo vya moto na wazalishaji, uzoefu unaonesha kwamba inapofikia hatua ya kupanda kwa bidhaa kutokana na sababu yoyote, bei za bidhaa huwa hazishuki. 

Mfano ni mwaka 2006 ulipo tokea ukame na kusababisha kupanda kwa bidhaa na bei ya umeme. Baada ya hali kutenge maa hakuna bidhaa iliyoshuka bei, hivyo wananchi waliende lea kuumia. Wito ni kwamba serikali kupi tia mamlaka zake, yanapotokea mambo ambayo yanasababisha kupanda kwa gharama za mai sha, ni vyema pia ikamjali mtu wa kawaida ambaye ni mtumi aji wa mwisho wa bidhaa au huduma badala ya kuendelea kuumia licha ya kuwapo mab adiliko.

 Kushuka kwa bei ya mafuta ni fursa tusiiharibu kwa kupandi sha bei za bidhaa nyingine bila sababu ,uchumi ukipata nafuu ,taifa zima linapata nafuu.