Nahodha wa zamani wa Manchester United inayoshiriki Ligi Kuu England (EPL), Rio Ferdinand, anatarajiwa kuwasili nchini kesho, imethibitishwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema nyota huyo wa zamani wa Timu ya Taifa ya England atafanya ziara ya ‘aina yake’ hapa nchini.
"Jumanne (kesho), ninatarajia kumshusha, Rio Ferdinand, nitafanya naye ziara kubwa hapa nchini itakayoweka historia," amesema Makonda.
Waziri huyo amesema malengo ni kuona wizara yake inakuwa bora zaidi kutokana na juhudi mbalimbali atakazozifanya.
Amesema atapambana ili kuona Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inafika mbali na kuwa mfano.
"Mpaka nimalize muda wangu kwenye wizara hii nitahakikisha inakuwa mfano na kila mmoja atatamani kufanya nayo kazi," Makonda amesema.
Ameongeza ujio utazidi kufungua milango ya Tanzania na kuwa kivutiio kwa wageni mbalimbali watakaokuja kutembea hapa nchini.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED