TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imesema kuna umuhimu maalum wa kusimamia sheria za haki jinai kwenye mnyororo wa taasisi zote zinazosimania haki jinai ili kulinda haki na usawa mbele ya wananchi.
Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Taasisi Haki Jinai kutoka THBUB, Constantine Mugusi, amebainisha hilo mbele ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
Amesema tume ina haki ya kusimamia wananchi na taasisi zote zilizo chini ya haki jinai kwa kuanzishwa kwa kitengo hicho machi 2025 kutokana na umaalum wake.
Mugusi amefafanua majukumu ya kitengo hicho cha haki jinai ni pamoja na kupokea malalamiko, kushughulikia, kuyachambua na kufanya kazi.
Kufatilia utendaji na uparesheni kuhakikisha utendaji wake unazingatia viwango vya haki za binadamu na utawala bora, usuluhishi na upatanishi.
Kufatilia utekelezaji wa mapendekezo ya tume kwa Tanzania bara Kifungu cha 29 kutoa tahadhari za mapema huenda mienendo inayoendelea ya utawala bora, ukiwamo ushauri wa namna ya kuepuka uvunjwaji na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora, kulinda usiri wa watoa taarifa wakiwamo waandishi wa habari na kuwahakikishia ulinzi, ili kulinda usalama wao.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED