Naibu Waziri wa Afya, Dk. Florence Samizi, amekitaka Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUCOHAS) kuendelea kuzalisha wataalamu wa afya wenye ubora, weledi na maadili ya hali ya juu, kukidhi mahitaji ya sekta ya afya nchini.
Dk. Samizi amesema hayo leo, Dar es Salaam, akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuboresha miundombinu na mazingira ya kufundishia na kujifunzia, ili wahitimu kupata ujuzi wa kisasa unaoendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia na huduma za matibabu duniani.
âKila mmoja anatakiwa kuwa balozi kwenye kampeni ya âJua Namba Yakoâ kwa kujitokeza kupima afya zao mara kwa mara, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kubaini mapema magonjwa yasiyoambukiza, shinikizo la damu na kisukari, na hivyo kuwezesha upatikanaji wa matibabu kwa wakati pamoja na kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.â
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Julieth Magandi, amesema MNH inaendelea kuhakikisha wanafunzi wa fani mbalimbali za afya wanapata mafunzo ya vitendo yenye ubora katika mazingira yanayowawezesha kujenga umahiri, weledi na maadili ya taaluma, ili wahitimu wawe tayari kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.
Mkuu wa MUCOHAS, Dk. Bonny Betson, amesema chuo hicho kitaendelea kuimarisha ubora wa mafunzo, tafiti na ubunifu ili kuzalisha wataalamu wenye umahiri, maadili na uwezo wa kukabiliana na changamoto za sekta ya afya nchini na kimataifa.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED