BAADHI ya wananchi wamesema elimu wanayoipata kuhusu matumizi ya gesi asilia imewapa uelewa mpana wa namna ya kutofautisha kati ya gesi inayotumika kwenye magari na inayotumika kwa ajili ya kupikia.
Wakizungumza katika banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), maarufu Sabasab, waliofika kupatiwa elimu hiyo, wamesema kwa sasa wameelewa tofauti Kati ya gesi asilia na gesi ya mitungi (LPG) inayotumika kupikia.
Wameeleza kuwa kupitia elimu hiyo pia wameelewa namna ya kutofautisha majukumu yanayofanywa na PURA, EWURA, pamoja na TPDC.
PURA inaendelea kushiriki na kutoa elimu kwa wananchi katika maonesho hayo.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED