Nchemba awashangaa wanaojadili kuhusu uchaguzi mkuu 2030

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 01:11 PM Jul 05 2026
Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba
Picha: Mtandao
Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, kuwafuatilia na kuwabaini watu wanaoendeleza mijadala kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2030 badala ya kujikita katika shughuli za maendeleo.

“Mkuu wa mkoa fuatilia wale wote ambao wanaendelea kuzungumzia uchaguzi uliopita tunataka tuwajue”, Waziri Mkuu, amemuagiza Kanali Mtambi.

Vile vile amesema: ''Tuna wananchi kiu yao ni kuona barabara. Sisi viongozi tunapata wapi muda? Kila wakati kwa makundi ya ‘Whatsapp’ ni kujadili uchaguzi wa 2030,” anasema Mwigulu.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Bunda, mkoani Mara, Dk. Nchemba amesema serikali haitaki kuona au kusikia mijadala ya kisiasa kuhusu uchaguzi wa mwaka 2030 kwa wakati huu, akisisitiza kuwa mjadala huo hauchangii juhudi za kuwahudumia wananchi na kuharakisha maendeleo.

“Kama sio ubinafsi ninini? Tuachane na mambo ya ubinafsi, tuelekeze huku kwenye mambo ya maendeleo,” amesisitiza.