Guardiola: City bado ipo mbio za ubingwa EPL

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 03:32 PM Mar 15 2026
Pep Guardiola
Picha: Mtandao
Pep Guardiola

Pep Guardiola amepaza sauti yake akiiambia Arsenal kwamba, mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England "hazijaisha" licha ya timu yake ya Manchester City kuwa nyuma kwa pointi 9 dhidi ya Washikabunduki hao, baada ya sare ya 1-1 ugenini dhidi ya West Ham juzi, iliyo hatarini kushushwa daraja.



Bado City wana mchezo mkononi dhidi ya Arsenal na wanatarajiwa kucheza nao Etihad mwezi ujao, kwa hiyo Guardiola alisisitiza kwamba, wao bado wa nafasi ya kushinda taji.

"Haijaisha," amesema Guardiola akiwaambia waandishi wa habari. "Hatukupoteza. Haijaisha. Tutaendelea.

"Ni vigumu sana, lakini tuna mchezo mkononi na mchezo huu nyumbani dhidi ya Arsenal. Sisemi utakuwa rahisi kuwashinda, lakini kuna matumaini."

"Sijui jinsi Arsenal wanavyocheza kwa sababu sikuona michezo iliyopita, lakini nina mambo machache ambayo nayapenda. Inaweza kuwa bora zaidi, lakini ndivyo ilivyo.

"Pointi tisa ni nyingi dhidi ya Arsenal, lakini tunapaswa kujaribu hadi mwisho. Kama haitawezekana basi tutawapongeza, lakini tunapaswa kujaribu."

CHANZO: ESPN