WAANDISHI wa habari wanaoandika habari za kupendelea serikali au wananchi, wameonywa wasijisahau na badala yake warejee kwenye nafasi yao sahihi ya kuwa daraja kwa pande zote.
Mwezeshaji mwelekezi wa taaluma ya habari ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF), Dastan Kamanzi, amebainisha kuwa uandishi wa tija ni muhimu kwa kuwa unaleta matokeo chanya yanayochochea maendeleo.
"Mwandishi anayesikika akitamba kuwa ameishughulikia serikali huyo hayupo sahihi,sisi siyo adui wa serikali wala wananchi bali ni daraja, habari za tija ndiyo zinapaswa kupewa kipaumbele kwa matokeo chanya," anasema Kamanzi.
Kamanzi ameyasema mwishoni mwa wiki wakati wa warsha maalumu kwa wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari, iliyoandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na International Media Support (IMS)
Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Kenneth Simbaya, amesema uandishi wa habari za tija utasaidia kuendelea kujenga uaminifu kwa wananchi lakini pia kujenga uwajibikaji kwa viongozi.
Amesema ndiyo maana wanasimamia mafunzo na kuona umuhimu wa kuendelea kuhamasisha uandishi wa habari wa aina hiyo.
âKatika zama hizi ambazo kuna taarifa za upotoshaji kwenye jamii, habari za tija ndiyo zenye nafasi nzuri ya kujenga jamii yenye uelewa, kuhamasishauwajibikaji pia kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihi ambazo pia zitasaidia katka kufikia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya taifa 2050,â amesema Simbaya.
Kwa upande wake Ofisa Programu wa IMS, Joyness Byarugaba, amesema mkakati wao ni kuweka juhudi za kuhakikisha mwanga unamulika mahali penye giza, ili kuleta mabadliko hasa kupitia kwenye sekta ya habari.
âTunaangaza vyombo vya habari kujitathimini kwa habari ambazo zinaripotiwa kupitia vyombo vyao, zinaleta chachu gani, wanahabari wawe na uelewa mkubwa katika kufanya kazi zao kwa maslahi ya umma, â amesema Joyness.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED