WAKALA wa Vipimo Mkoa wa Morogoro umewataka wafanyabiashara kuzingatia matumizi ya vipimo vilivyoidhinishwa na kuachana na makopo, ndoo za plastiki na visado, ambavyo havitambuliki kisheria katika upimaji wa bidhaa.
Meneja wa Wakala huo mkoani Morogoro, Deogratias Hussein, anatoa rai hiyo wakati wa kugawa mizani kwa wafanyabiashara wa Soko la Mboga, Feri Magole wilayani Kilosa.
Amesema matumizi ya vipimo visivyo rasmi yanaweza kusababisha udanganyifu na kuathiri haki za walaji pamoja na wafanyabiashara wenyewe, hivyo mamlaka yake itaendelea mamia utekelezaji wa sheria za vipimo.

Mwenyekiti wa Soko la Mboga Feri Magole, Mohamed Said, amesema kuwa ugawaji wa mizani unaongeza uwazi katika biashara na kusaidia kuondoa changamoto za vipimo visivyo rasmi.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED