Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema makubaliano ya kumaliza vita vya Iran yamejadiliwa kwa kiasi kikubwa na maelezo yatatangazwa hivi karibuni.
Katika chapisho kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump amesema makubaliano hayo yatajumuisha kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz.
Asubuhi ya leo, shirika la habari la Iran la Tasnim, limesema kuwa Mlango wa Bahari utarejea katika viwango vya kabla ya vita ndani ya siku 30.
Na kwamba makubaliano huenda yakasimamisha mashambulizi pande zote. Muda mfupi ujao tunatarajia tamko kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, kufuatia mkutano wake na waziri wa mambo ya nje wa India mjini New Delhi - unaweza kufuatilia moja kwa moja hapo juu pindi atakapoanza.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei, ameiambia televisheni ya taifa jana, kuwa, wawakilishi wa Marekani na Iran, wamekuwa wakikutana katika wiki za hivi karibuni.
Lakini ameonya hilo haimaanishi kuwa makubaliano yatafikiwa katika masuala muhimu na kuwashutumu wamarekani kwa kutoa "taarifa zinazokinzana".
Trump pia amesema alikuwa na "mazungumzo mazuri" na viongozi wa Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar, na wengine kuhusu "Mkataba wa Maelewano unaohusu AMANI".
Chanzo: BBC
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED