Serikali ya Sierra Leone, imekubali kupokea mamia ya wahamiaji kutoka Afrika Magharibi, wanaofukuzwa kutoka Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje, Timothy Kabba, amesema makubaliano hayo yatawezesha Sierra Leone kupokea hadi watu 300 kwa mwaka kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Magraribi (ECOWAS), huku kiwango cha juu kwa mwezi kikiwa watu 25.
Ndege ya kwanza inatarajiwa kuwasili Mei 20, 2026 ikiwa na wahamiaji 25 kutoka Senegal, Ghana, Guinea na Nigeria.
Hatua hiyo ni sehemu ya sera ya utawala wa Rais Donald Trump ya kuongeza kasi ya kuwafukuza wahamiaji.
Hata hivyo, mashirika ya haki za binadamu na wataalamu wa sheria wameendelea kuhoji uhalali wa kuwapeleka wahamiaji katika nchi ambazo si za uraia wao.
Serikali ya Sierra Leone haijaeleza iwapo wahamiaji hao wataruhusiwa kuishi nchini humo au watarudishwa katika nchi zao za asili.
Chanzo: DW
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED