Meli kupita kwa kiwango cha awali huenda kuanza siku 30 zijazo

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 12:10 PM May 24 2026
Mlango wa Hormuz
AI
Mlango wa Hormuz

Shirika la habari la Iran la Tasnim, linaripoti kwamba ingawa Mlango wa bahari wa Hormuz hautarejea katika hali yake ya kabla ya vita, idadi ya meli zinazopita inaweza kurudi katika viwango vya kabla ya vita, ndani ya siku 30.

Hiyo ni kutokana na makubaliano kati ya Marekani na Iran, Mlango wa bahari wa Hormuz.

"Hautarejea katika hali yake ya kabla ya vita" kimenukuliwa chombo hicho cha habari, Tasnim.

Chombo hicho cha habari kilicho na uhusiano na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), kimekuwa kikiripoti maelezo yaliyomo kwenye makubaliano hayo na Marekani asubuhi hii, lakini Marekani haijathibitisha kuhusu maelezo ya makubaliano yoyote.

Hata hivyo, inaongeza kuwa Iran "inasisitiza kutumia mamlaka yake kuhusu uamuzi huo".

Inaongeza kuwa kizuizi cha majini cha Marekana dhidi ya meli zinazoingia na kutoka bandari za Iran lazima "kuondolewa kabisa" ndani ya siku 30.

Chanzo: BBC