Kihongosi ageuka mbogo watumishi wa umma kutohudhuria mikutanoni

By Halfani Chusi , Nipashe Jumapili
Published at 09:56 AM Jun 21 2026
Kihongosi ageuka mbogo watumishi wa umma kutohudhuria mikutanoni
PICHA: Halfan Chusi
Kihongosi ageuka mbogo watumishi wa umma kutohudhuria mikutanoni

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CCM Kenani Kihongosi amekemea vikali baadhi ya viongozi wa umma kutohudhuria mikutano ya chama akisistiza jambo hilo linafanya uatatuzi wa kero uwe mgumu.

Kihongosi alitoa karipio hilo jana wakati akiwahutubia wananchi wa mkoa wa Iringa katika Viwanja vya Mwembetogwa na kusisitiza tabia hiyo haivumiliki. Akiwa mkutanoni hapo alipokea kero ya mfanyabiashara wa mbao aliyekuwa na deni benki la Sh. milioni 1.7 ambaye alidai sababu ya kudaiwa kwake ni mfanyabiashara wa fenicha, Mandela Furniture, amemzulumu. “Mimi ninakuja kuongea hapa kwa sababu yeye kesi yake mkuu wa mkoa anaijua. Nahitaji fedha kutoka kwa mkurugenzi ambaye alipitia kwa Mandela. Wakachukua hela, wakatengeneza fenicha za serikali tangu mwaka juzi. Nilikuwa nimechukua mkopo benki wa milioni tano, mbao nilizowapa zina thamani ya milioni Sh. milioni 1.7.”

 Baada ya kumsikiliza, Kihongosi alianza kwa kuuliza: “Mwanasheria halmashauri yupo?” Akajibiwa ‘hayupo’. “Hili jambo litaleta picha mbaya naweza nikafanyika uamuzi mbaya halafu mkaanza kuleta lawama.

 â€œMimi sijaja hapa kucheza, wala kucheka na mtu. Maana yake hapa ni kwamba serikali inanilazimisha nikwame kazi. Hii ilikuwa inajulikana kama itafanyika lini, watu kwa kuamua hawajaja. Sasa mimi ninaweza nikaahirisha mkutano kwa sababu wajibu wa hoja hawapo.

 â€œHaya mambo ndio huwa yanafanya baadaye wananchi mtasikia wanasema wanaonewa. Hapa kuna watu wana shida inabidi waje wajibu shida hizo za watu. Wameamua kujipa majukumu yao. Niombe tu mkuu wa wilaya mwambie mkurugenzi na wakuu wa idara wote: matatizo ambayo hayatajibiwa hapa tukutane hotelini. Tena mimi ninaenda kulala Ruaha Mbuyuni, watakuja huko ndio tutaenda kufanya sasa hayo maamuzi. Hatuwezi kucheka cheka na watu hapa kwa sababu vitu hivi vinakwaza.

 â€œYaani DC yupo, mkuu wa idara hayupo? Mwanasheria yuko wapi ambaye ana udhuru wake ni nani? Mama wewe usipate shida, sawa nenda kanisubiri pale kwenye jukwaa, pale nenda ukanisubiri pale. Na ninataka viongozi wote waje hapa. Sitoki hapa mpaka wafike wote waje. Hata kama tutakaa ni usiku, waje hapa hapa,” alisema kwa ukali Kihongosi.

 Pia alipokea kero ya dereva ambaye alipokwenda kuhuisha leseni yake alipunguziwa madaraja kwa kuwa amezidi umri wa miaka 60 kwamba hawezi tena kuendesha gari. Kihongosi alimwagiza OCD amsikilize na atatue shida yake.

 Kuhusu ombi la viziwi kusafiri kwenda Moshi katika siku ya viziwi duniani, waliohitaji Sh. 1,050,000:

 Kihongosi alimsukumia suala hilo mbunge wa jimbo “Mbunge wenu si yupo? Wananchi au nyinyi mnasemaje afanye asifanye? Wangapi mnasema hili jambo mbunge amalize hapa hapa! Ebu punga mkono namna hii. Haya Mbunge (Fadhili Ngajiro) kabla sijashuka, uwe umewapatia. Safi amesema analeta sasa hivi wabunge majembe wapo! Nenda dada uchukue kabisa.” Alisuluhisha kihongosi