Serikali yaweka mazingira tulivu uwekezaji, ikiondoa kanuni 374

By Christina Mwakangale , Nipashe Jumapili
Published at 08:03 PM Jun 14 2026
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo
Picha: Mpigapicha Wetu
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo, amesema serikali imehakikisha kuna mazingira tulivu ya uwekezaji, kwa kuweka masharti ya kikodi ambayo ni rafiki, huku ikiondoa kanuni zilizokuwa kikwazo zaidi 370.

Londo amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati utambuzi wa kampuni bora 100 za chapa za Afrika zinazotengeneza bidhaa zilizoko barani humo, jijini Dar es Salaam.  

Amesema kwamba pia bajeti ya fedha kwa mwaka 2026/2027 imekuwa ya kwanza katika kuanza utekelezaji Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, huku kwa asilimia 70 ikitegemea utendaji kazi wa sekta binafsi.

“Tunatambua mchango wa sekta binafsi, watoa huduma na serikali inaunga mkono juhudu hizo za watanzania na wanakuwa washiriki wa kweli katika mnyororo wa thamani,” amesema.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo, akiwa na wadau mbalimbali wa tuzo hizo
Mratibu wa tuzo hizo, Deogratius Kilawe, amesema kwamba lengo la kuandaliwa kwa tuzo hizo ni kutengeneza ushindani wa soko kwa bidhaa za Afrika, na kuongeza huduma bora kwa wananchi.

“Mwaka wa nne tunawatambua wazalishaji hao sasa, watu walioshiriki kuwania ni takribani 5,000 hadi kufikia mchakato wa kampuni 500, kutoka katika nchi zaidi ya saba,” amesema Kilawe.